Alhamisi, 30 Machi 2017

ALICHOONGEA NEY WA MITEGO BAADA YA KUACHIWA NA POLISI.


Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kuliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Nay wa Mitego ambaye alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za wimbo wake wa ‘WAPO’ kutokuwa na maadili, Nay wa Mitego ametoka kituoni hapo leo March 27 2017.

Jumatatu, 27 Machi 2017

PROFESA JAY AKANA KUMCHANA AFANDE SELE KWENYE KIBABE.

Jay anatuhumiwa kuandika mstari ambao unaonekana kumgusa Afande kwenye wimbo huo. “Usipo nisikia leo ujue kesho narudi, mwambieni mfalme wenu siti yangu aifute vumbi,” amerap Profesa kwenye wimbo huo.
Akiongea na E News ya EATV, rapper huyo amekana kwa kusema, “Afande Sele mimi ninamheshimu toka yupo Chadema kabla hajaenda ACT na hata wakati tunaanza harakati za kugombea kila mmoja alimtakia mwenzake kila la kheri.”

TAARIFA YA SPIKA WA BUNGE NDUGAI NA WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGEBAADA YA KUTEMBELEA TPA. TPA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alifanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam, TPA kwa lengo la kukutana na mamlaka hiyo ili kupata maelezo ya kina juu ya makontena yenye mchanga wa dhahabu yanayoshikiliwa na mamlaka hiyo yaliyokuwa yasafirishwe nje ya nchi.

NMB YAWAWEZESHA WATEJA WAKE KUTUMA PESA KWENDA BENKI NYINGINE KUPITIA NMB MOBILE.

Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada katika Benki ya NMB, Stephen Adili akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani)
Akizungumza katika hafla ya kuitambulisha huduma hiyo Adili alisema, Huduma hii inakuja kumaliza tatizo la wateja kutumia muda mwingi kwenye mchakato wa kuhamisha fedha. Muda ni mali na kwa kulitambua hilo, tumekuja na huduma hii ambayo inafanyika popote, hata ukiwa ufukweni unapunga upepo.”

RAIS AMEAGIZA MSANII NAY WA MITEGO AACHILIWE HURU KWANI HATA YEYE WIMBO HUO AMEUPENDA.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amedai kuwa Rais Dkt John Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Nay wa Mitego.“Yaani asiondoe kitu chochote, ila aongeze kwasababu unaelezea changamoto zilizopo kwenye jamii halafu wanaitikia watu ‘wapoo’” amesema Dkt Mwakyembe kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma leo

TAIFA STARS KUIKARIBISHA BURUNDI KESHO UWANJA WA TAIFA.

Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras ‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.
Katika mchezo huo wa Jumamosi, Taifa Stars ambayo kwa sasa inanolewa na Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata ambao ni makocha wapya wa kikosi hicho, walishinda kwa mabao 2-0.

RAIS MAGUFULI AWAPANDISHA VYEO MAOFISA WA UHAMIAJI.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, kupandishwa vyeo na uteuzi huo umeanza tangu Februari 28, mwaka huu.
Aliwataja walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka na Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia.

JWTZ LAKIRI KUDAIWA BILIONI 3 NA TANESCO, KUANZA KUPUNGUZA DENI HILO LEO

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akiongea na wanahabari Jumapili hii ambaye alibainisha wazi kuwa tayari Tanesco wamelipatia jeshi notisi ya kukatiwa umeme katika vituo vyake vyote leo, endapo deni hilo lisipolipwa.
“Hivi karibuni tumepokea taarifa ya Tanesco kuhusu kusitisha huduma kwenye vituo vyetu vyote kesho (leo) kutokana na deni kubwa tunalodaiwa. Hii ni kutokana na agizo la Rais John Magufuli kwa shirika hilo, kuwa liwakatie huduma wale wote wanadaiwa na shirika hilo, tunadaiwa kiasi kinachozidi kidogo bilioni 3 na Tanesco peke yake ” alifafanua Jenerali Mabeyo.
“Tayari nimeagiza watendaji wetu watafute kiasi cha Shilingi bilioni moja ili kesho (leo) hundi ipelekwe haraka Tanesco kwa ajili ya malipo, na kuzuia tusikatiwe umeme,” alieleza.
Aidha Mabeyo alibainisha kuwa pamoja na deni hilo la Tanesco, pia JWTZ inadaiwa na wazabuni wengine wanaotoa huduma kwao na tayari Hazina imeanza kulipatia jeshi hilo fedha kidogo kidogo ili kupunguza madeni hayo tuna imani tutayamaliza katika muda mfupi ujao kwasababu tayari serikali imeanza kutekeleza hilo.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA KUMWAKILISHA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN TAMASHA LA PASAKA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akitangaza mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 16 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Msama amemtaja Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba kuwa ndiye atakuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

PROF. MBARAWA: NEEMA YAJA WAFANYABIASHARA KANDA YA ZIWA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akielekea kukagua Bandari ya Kemondo mkoani Kagera ili kujionea utendaji kazi wake.  Kulia ni Meneja wa Bandari Kanda ya Ziwa, Bw. Abel Moyo.

IGAD;WAKIMBIZI WAHIFAHIDHIWE KWA MUJIBU WA SHERIA ZA KIMATAIFA

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn

ZANTEL YAZINDUA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI WA 4G NA HUDUMA ZA KIBENKI KWA NJIA YA SIMU KISIWANI PEMBA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin akizungumzawakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. KushotoniMkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha.Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.

PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.

WOTE MNAKARIBISHWA KUSHIRIKI JUKWA HILI APRILI 11-12, 2017


Hakuna kiingilio.
Kuna ukomo wa nafasi. Jiandikishe kupitia ukurasa huu, kwa kuchagua hapo chini kulia ' Going' au hata ' Maybe' kama huna hakika. Au kwa kutembeleahttp://www.tzdiaspora.org